Thursday, 22 August 2013

NISENE UA NISISEME....

 
 
 
 
kILIMANJARO
SERIKALI YA RAIS MRISHO JAKAYA KIKWETE BADO IMEKAA
 KIMYA KUZIBITISHA
 URAIA WA MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA.
 


Uraia Africa

Hivi karibuni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu Mrisho Jakaya Kikwete alimfuta kazi msajili wa vya vya siasa ndugu John Tendwa na kumteuwa msajili mpya ndugu Francis S.K Mutungi.

Hata hivyo habari ambazo gazeti hili limezipata zinasema uraia wa msajili huyo una utata kwa vile siyo raia wa Tanzania bali ni raia wa kenya. Hali hii inakuwa tata kwa sababu nchini kwetu tumezungukwa na nchi mbalimbali na kwa sababu nchi yetu ni yenye amani na haina ubaguzi wageni wengi wamekuwa wakiingia kupitia njia za panya na kujifanya wao ni watanzania,.......hawa watu wanaghalamiwa na serikali yetu kama ni watanzania tangu shule za msingi hadi vyuo vikuu, sasa unaona wanaanza kupewa nyazifa kubwa kubwa, kuna hatari ya kuja kupata rais wa nchi kutoka nchi jilani kama hali ya kuzibiti wageni haitapewa uzito wa kusitahili.

Naye mkazi wa Ibwera, Mwemage kati mkoani kagera ndugu Sweetbert Mshobozi amesifia hatua ya hivi karibuni ya rais kikwete kuwaambia wageni wote warudi makwao kwa vile wametuvuna vya kutosha, ingawa aliongeza sensa ya kuwajuwa wahamiaji haramu ingeanzia kwa viongozi wa juu wa kitaifa kwa vile anaimani kuna wabunge, mawaziri amabo siyo raia wa Tanzania lakini wamejichokomeza na kujiita watanzania.
Zigua Simo na Njero
 

No comments:

Post a Comment