Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeishutumu serikali ya Rwanda kwa
kuwaunga mkono wapiganaji wa kundi hilo la M23, tuhuma ambazo
zimendelea kukanushwa na utawala wa Kigali.
Hata hivyo Msaidizi
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amenukuliwa akisema wapiganaji wa
kundi la waasi wa M23, wameonekana wakirusha makombora wakilenga Rwanda.
Kwa mujibu wa habari za uchunguzi za UN ni kwamba wengi wa wapiganaji
wa M23 ni wanajeshi walioasi jeshi la serikali ambao wengi wao ni wa
kabila la Kitutsi sawa na uongozi wa Rwanda.
Bwana Ban Ki-moon,
alizungumza na rais Paul Kagame baada ya serikali ya Rwanda kuishutumu
Congo, kwa kufanya shambulio katika ardhi yake makusudi na kumuua mama
mmoja na kumjeruhi mtoto wake.
Kufuatia kutuhumiwa kwa Rwanda
kujihusisha na kuwasaidia waasi wa DRC, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki-moon ametoa wito kwa Rais wa Rwanda kuacha kufanya vitendo
vinavyochochea vita huko DRC kwani anazidisha uhasama kati ya nchi yake
na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambalo litahatarisha
amani ya nchi za maziwa makuu.
Serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa zimeishutumu serikali ya Rwanda kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa kundi hilo la M23, tuhuma ambazo zimendelea kukanushwa na utawala wa Kigali.
Hata hivyo Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amenukuliwa akisema wapiganaji wa kundi la waasi wa M23, wameonekana wakirusha makombora wakilenga Rwanda.
Kwa mujibu wa habari za uchunguzi za UN ni kwamba wengi wa wapiganaji wa M23 ni wanajeshi walioasi jeshi la serikali ambao wengi wao ni wa kabila la Kitutsi sawa na uongozi wa Rwanda.
Bwana Ban Ki-moon, alizungumza na rais Paul Kagame baada ya serikali ya Rwanda kuishutumu Congo, kwa kufanya shambulio katika ardhi yake makusudi na kumuua mama mmoja na kumjeruhi mtoto wake.
Kufuatia kutuhumiwa kwa Rwanda kujihusisha na kuwasaidia waasi wa DRC, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa Rais wa Rwanda kuacha kufanya vitendo vinavyochochea vita huko DRC kwani anazidisha uhasama kati ya nchi yake na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambalo litahatarisha amani ya nchi za maziwa makuu.
No comments:
Post a Comment