Monday, 2 September 2013

AMINATA TOURÉ AWA WAZIRI MKUU SENEGAL

ATC....
 
AMINATA TOURÉ AWA WAZIRI MKUU SENEGAL

Aminata Touré (Pichani), waziri wa zamani wa sheria katika Serikali ya Senegal, ameteuliwa kushika wadhifa wa Waziri Mkuu wan chi hiyo. Uteuli huo umefanya na Rais Macky Sall wa Senegal masaa tu baada ya kumtoa kazini Adbou Mbaye aliyemteua aliposhika madaraka mwaka jana.

Aminata Touré, aliiambia redio ya taifa ya Senegal kwamba amepokea uteuzi huo kama heshima kubwa kwake, wanawake wenzake na wananchi wote wa Senegal. Aidha, alisema amekubali amri ya rais ya kuunda serikali mpya.

Bi Touré atakuwa mwanamke wa pili kuwa waziri mkuu nchini Senegal - baada ya Madior Boye, aliyeshika wadhifa huo kwa miezi 18 mwaka wa 2001.

Bwana Sall alimshinda Rais Abdoulaye Wade katika uchaguzi wa rais uliofanyika Machi 2012, akiahidi kupambana na umaskini na rushwa. 

Aminata Touré (Pichani), waziri wa zamani wa sheria katika Serikali ya Senegal, ameteuliwa kushika wadhifa wa Waziri Mkuu wan chi hiyo. Uteuli huo umefanya na Rais Macky Sall wa Senegal masaa tu baada ya kumtoa kazini Adbou Mbaye aliyemteua aliposhika madaraka mwaka jana.

Aminata Touré, aliiambia redio ya taifa ya Senegal kwamba amepokea uteuzi huo kama heshima kubwa kwake, wanawake wenzake na wananchi wote wa Senegal. Aidha, alisema amekubali amri ya rais ya kuunda serikali mpya....See more

No comments:

Post a Comment