Monday, 2 September 2013

Mwili wa shujaa....Jeshi la Wananchi wa Tanzania

Zigua simo na njero
Mwili wa shujaa huyo uliagwa jana katika Viwanja vya Jeshi la
 Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dar es Salaam.

Wanajeshi wa M.23
Waziri wa Mambo ya Nje
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kitaifa, Bernard Membe, ameongoza mamia ya waombolezaji katika kuaga mwili wa mwili wa Meja Khatib Mshindo aliyefariki dunia   Agosti  28, mwaka huu baada ya kuangukiwa na bomu  huko Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC). Bomu lililomuua ofisa huyo wa JWTZ aliyekuwa katika misheni ya Umoja wa Mataifa ya Kulinda Amani, lilipuliwa na waasi wa M23.
Kifo cha ofisa huyo kimekuja  siku 47 tangu kuuawa kwa bomu, wapiganaji wengine saba wa Tanzania  huko Darfur.
Wapiganaji hao walishambuliwa na  kundi linaloaminiwa kuwa la Janjaweed.
Maombolezo ya jana yalifanyika katika Viwanja vya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na  viongozi mbalimbali wa JWTZ.
Wanajeshi wa M.23
 Akitoa Salam za rambi rambi, Waziri Membe alisema taifa limempoteza shujaa aliyekuwa akitekeleza majukumu yake nchini DRC.
 “Tumempoteza mtu shujaa, alikuwa akitekeleza majukumu yake nchini DRC, Serikali haitaweza kumsahau, kwa sababu alikuwa miongoni mwa mashujaa waliokufa kazini,” alisema Membe.
Alisema kifo hicho kimeifanya taifa kumwaga damu ya kishujaa na kwamba waliobaki hawarudi nyuma na badala yake, watakuwa na ari ya kusonga mbele katika mapambano.  “Waliobaki wataendelea kushika mpini kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa nchi hiyo ambao wamekata tamaa ya maisha kutokana na vita vinavyoendelea katika nchi yao,” alisema.
Waziri huyo alisema watu wanaoathirika katika nchi zenye vita ni wanawake na watoto.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange alisema, marehemu alifariki dunia akiwa njiani wakati akiwahishwa hospitalini.
 Alisema waasi wa M23 walirusha bomu lililosababisha kifo cha  marehemu na kujeruhi watu wengine watano ambao mpaka sasa wanaendelea na matibabu.
Jenerali Mwamunyange alisema JWTZ litaendelea kuwakumbuka marehemu hao na kuwaombea majeruhi ili waweze kupona haraka na kurejea kwenye majukumu yao  Alisema kuwa, marehemu alikuwa akifanya kazi katika  kikosi cha mizinga 83 KJ kilichopo Kibaha Pwani. Mwili wa marehemu ambaye ameacha mjane na watoto watatu, umesafirishwa kwenda Zanzibar kwa ajili ya maziko.

Mnazi wa ajabu
KIKUNDI cha waasi cha M23 kinachopambana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kimeripotiwa kupigwa vibaya na kutikisa nguvu za kikundi hicho kutokana na baadhi ya wapiganaji wake kuripotiwa kupoteza maisha.
  
Mapigano baina ya M23 na Jeshi la Serikali ya DRC linalosaidiwa na Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), yameibuka upya ndani ya wiki hii.
  
Habari za kiintelijensia  zinasema kuwa, kutokana na shambulio hilo, Serikali ya Rwanda imelazimika kuingilia kati kusaidia waasi hao kwa kupeleka bataliani mbili zenye jumla ya askari 1,700 huko DRC, ili waweze kukabiliana na nguvu ya majeshi ya JWTZ, DRC, Monusco na Brigedi ya Majeshi ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa yenye mamlaka ya kujibu mapigo (FIB).

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Rwanda imepeleka bataliani hizo mbili zenye askari 850 kila moja saa 48 zilizopita na kwamba wamevuka mpaka kuingia DRC katika eneo la Kibumba, lakini wanashindwa kusonga mbele.
  
Habari zaidi zinasema sababu ya Rwanda kupeleka askari wake hao ni kusaidia M23 ambao walipigwa sana Agosti 23 na 27, mwaka huu katika eneo la vilima vya Kibati na  kuikimbia ngome yao.
  
“M23 walitandikwa sana Agosti 23 na 27 katika eneo la vilima vya Kibati, na kulazimika  kuikimbia ngome yao, ndio maana sasa hivi Rwanda imepeleka batalioni zao kuwapa nguvu, lakini wanashindwa kusonga mbele maana hawajielewi kwa sababu ya kipigo walichopata,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
  
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, eneo la Kibati ndilo eneo kubwa la M23 ambalo wamekuwa wakitumia kuhifadhi silaha zao za kivita, lakini wakati wa mapambano majeshi ya JWTZ , DRC, MUNUSCO na FIB yalisambaratisha kabisa ngome hiyo ya waasi.
  
FIB inaundwa na askari wengi wa Afrika Kusini na Tanzania. Habari zaidi zinasema kwa sasa majeshi ya DRC, Monusco na FIB yanawasubiri kwa hamu askari hao wa Rwanda kuingia uwanja wa vita ili kukabiliana nao kama walivyokabiliana na waasi wa M23.
  
“Taarifa tulizonazo hivi sasa Rwanda inajiuliza iwapo isonge mbele kupambana au irudi nyuma, ikifikiria pia kipigo walichopata M23,” kilisema chanzo kimoja cha habari. 

Inaelezwa kwamba, kutokana na kipigo walichopata M23 siku chache zilizopita kimepelekea Rwanda kujikuta ikikiri na kusema ukweli juzi kuwa inakisaidia kikundi hicho cha waasi. - See more at: http://williammalecela.blogspot.com/2013/09/rwanda-yapeleka-wanajeshi-1700.html?spref=fb#sthash.68JFL4wX.dpuf

No comments:

Post a Comment