Tuesday, 3 September 2013

RWANDA YAPANDISHA USHURU KWA MAGARI YENYE USAJILI WA TANZANIA



Zigua Simo na Njero


Ramani Ya Rwanda

Katika hatua ambayo inaonyesha maana ya kauli ya Rais KAgame wa Rwanda kuwa anajua namna ya kuiadhibu Tanzania, Serikali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara (ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo (Fuel and Dry Cargo) yenye namba za usajili za Tanzania yanayovuka mpaka wa Rusumo kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Taarifa za kuaminika zinasema kwa siku moja zaidi ya magari 350, yakiwemo malori na gari ndogo, yanavuka mpaka wa Rusumo ambapo zaili ya asilimia 60% ya magari hayo yana namba za usajili za Tanzania.

Wamiliki wa Malori wa Tanzania wameiomba serikali kuingilia kati ili kunusuru hali hiyo.




 ...........................................
>NUKUU:
" Hao wahamiaji haramu hasa wale wa Rwanda wasihusishe hatua ya kuwaondoa nchini na mgogoro wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda,Tanzania ni nchi yenye sheria zake hivyo lazima ziheshimiwe na mataifa mengine"
 ..............................................
 
KIBOKO..TZ



No comments:

Post a Comment