Chui |
Hili huwatokea watu katika fani au tasnia mbalimbali mfano siasa, uanaharakati, mchezo wa soka, filamu na maigizo.
Ndivyo ilivyo kwa Amri Athumani maarufu King Majuto, ambaye ni mwingizazi na mchekeshaji maarufu nchini anayetambulika na kutajwa
kirahisi hata na watoto katika Tanzania hata nje ya mipaka yake.
Kwa maelezo yake, King Majuto amekuwa mwigizaji wa
vichekesho kwa miaka 55 sasa, akijivunia mafanikio makubwa na
kutambuliwa hata kimataifa.
Umaarufu wake ndiyo uliomsukuma mwandishi wa
makala haya kufunga safari hadi eneo la Donge mkoani Tanga yalipo
maskani ya Majuto ambaye hata ukimwona tu unaweza kucheka kutokana na
vituko vyake vingi vyenye kuvutia na kufurahisha.
Alivyoanza kuigiza
Majuto anaeleza alivyoanza kuigiza akisema:
“Nilianza kuigiza mwaka 1958 nikiwa na umri wa miaka 10. Nilikuwa darasa la pili, Shule ya Msingi ya Msembweni mkoani Tanga, kuna siku tukiwa darasani mlevi mmoja alikuwa akipita karibu na shule yetu, huku akipiga ngoma kwa nguvu.”
“Nilianza kuigiza mwaka 1958 nikiwa na umri wa miaka 10. Nilikuwa darasa la pili, Shule ya Msingi ya Msembweni mkoani Tanga, kuna siku tukiwa darasani mlevi mmoja alikuwa akipita karibu na shule yetu, huku akipiga ngoma kwa nguvu.”
Anaongeza:”Mwanafunzi mmoja akajiunga kucheza huku
mlevi yule akizidi kusogea na kuongeza mdundo, mwalimu aliyekuwa
akifundisha alikasirika na kumtuma mwanafunzi mwingine kumfukuza yule
mlevi, lakini badala ya kumfukuza mlevi na kumwita mwanafunzi anayecheza
naye akajiunga kucheza.”
Anasema kuwa mwalimu alivyoona hivyo, alitoka nje
ya darasa kwa kishindo na kwenda kumfukuza yule mlevi, lakini cha
kushangaza wakati mwalimu alipomkaribia yule mlevi alianza kutingisha
mabega yake kufuatisha mdundo ya ngoma, badala ya kumfukuza mlevi naye
alijiunga na kuanza kucheza.
“Baada ya dakika tano kama shule nzima ilikuwa
ikicheza ngoma, na baada ya hapo niliazimia kuwa msanii kwa kuwa sanaa
ilimlainish hata mwalimu wetu aliyekuwa mkali kupita kiasi,” anasimulia
Majuto.
Anaongeza kuwa mwaka 1966 alimaliza darasa la nane
na mwaka uliofuatia alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambapo
walikuwa wakilipwa Sh20 na kufanya kazi hadi mwaka 1970, alipolazimika
kuacha kwa sababu alikosa nafasi ya kufanya sanaa kama ndoto zake
zilivyokuwa zikimtuma tangu utotoni.
Utamaduni |
No comments:
Post a Comment