WAHAMIAJI HARAMU WAONDOKA NCHINI TOA MAONI JINA NA MAHALI
|
Nyayo |
|
Kinyago |
|
Nguchiro |
Zoezi la usalimishaji wa silaha na kuondoka nchini kwa wahamiaji haramu limezidi kushika hatamu katika mkoa wa kagera.
Katika mpaka wa rusumo mkoani Kagera mamia ya wahamji haramu
wameonekana kwa wingi wakiingia nchini Rwanda huku hofu ya visasi
miongoni mwa jamii zao ikizidi kudhirika.
Mkuu wa mkoa wa
Kagera Kanali Mstaafu Fanbian Masawe amethibitisha kuwa mpaka hivi sasa
zaidi ya wahamiaji haranu elfu kumi wameondoka nchini huku zaidi ya
silaha 60 zikisalimishwa.
Taarifa ya mwandishi wetu Mariam Emily kutoka mkoni Kagera mpaka wa Rwanda na Tanzania Rusumo inasomwa studio.
Ukifa Katika mpaka wa Tanzania na Rwanda Rusumo mkoani kagera moja kwa
moja unaweza dhani idadi kubwa ya watu hawa ni wakimbizi wanao ingia
nchini Rwanda.
Wengi ya watu hawa wameishi Tanzania kwa miaka mingi bila kuwa na vibali maalumu vya makazi.
Wamekili kuitika wito wa rais kikwete wa kuondoka kwa ihari, lakini
hofu yao kubwa ni visasa dhidi ya wenzao wa Rwanda ambao waliathirika na
vita vya haraiki vya mwaka 1994.
Wengi ya wahamiaji wanadai kuwa zoezi hili ni halali, lakini majaliwa ya maisha yao nchini Rwanda yanabaki kuwa kitendawili.
Kukithiri kwa vitendo vya ujambazi na ukatili miogoni mwa jamii
kumeisukuma serikali kuendesha zoezi hili linalo tazamwa kama ahueni ya
matukio ya mtio huu nchini.
Agizo la kuwataka wahamiaj haramu
wote kuondoka nchini na kusalimisha silaha haramu lilitolewa na Rais
JAKAYA KIKWETE akiwa katika ziara yake Mkoani KAGERA ,ambapo alisema
hatua hiyo ni wajibu wa nchi kulinda mipaka yake na hailengi kuchochea
uhasama na nchi jirani na TANZANIA.
|
Wanyama |
No comments:
Post a Comment